top of page
Фото автораНика Давыдова

Flashback: President Kenyatta and Jaramogi Oginga Odinga duel during Kenyatta’s speech in Kisu

Na mimi naanza na msemo wa Kiswahili usemavyo kwamba, asanti ya punda ni mateke.

(Cheers from supporters and boos from crowd)

Asanti ya punda ni mateke.

Tunakuja hapa kuwaletea bahati, kuwaletea hospitali ambayo ni ya kutibu wananchi.

Na kuna vinyangarika, vinyangarika wa KPU wanadhubutu kuja hapa na kusemasema maneno machafu machafu.

Mimi ninafurahiwa sana kuwa na rafiki yangu Odinga ambaye ndiye muongozi wa hawa watu, yuko hapa.

Na mimi ningesema

(Interupter:  ‘sisemi’)

Mimi ningesema, kama si heshima ya urafiki wetu na wewe Odinga, mimi ningesema utiwe nguvuni leo (boos from the crowd).

Tuangalie ni nani anatawala, ni nani anatawala nchi hii, kama ni KANU ama ni vinyangarika wengine wanatawala nchi hii.

Walakini, mimi nasema kwamba, kama hawa watu wako wachafu, kama wakitoa nyokonyoko, sisi tutawaonyesha kwamba Kenya iko na serikali yake

(Cheers from supporters and boos from crowd).

Hatuwezi kuchezewa sisi, na wewe bwana Odinga unajua mimi sina machezo, nimekuacha siku nyingi kwa sababu wewe ni rafiki yangu, kama si hivyo wewe unajua mimi ningefanya nini.

(Interupter ‘tupa yeye ndani’)

Apana kazi yako kuniambia nitupe wapi, mimi najua mwenyewe, mimi najua mwenyewe (laughing). Labda wewe usemae naweza kutupa wewe ndani ya Manyani kuliko rafiki yangu (Manyani was a detention camp, now a jail)

Kwa hivyo mimi nasema hivi ndugu zanguni, ni lazima, ni lazima tujue kwamba hii ni nchi ya Kenya, ambayo, inajitawala yenyewe, ambayo, ina madaraka ya wananchi.

Na hatuwezi kukubali hata kidogo, hatuwezi kukubali hata kidogo, mtu, au vikundi vya watu, kutuchezea.

Kama Odinga ujuavyo wewe, tulikuwa na wewe pale, mimi nilikwambia kwamba, mimi ntaangusha Ngereza, nilisema hivyo, sikusema? Kasema tutawaangusha.

Itakuwaje vinyangarika hapa unawaweka kidogo kidogo tu? Kuja kucheza na serikali hapa.

Na kwa hivyo leo mimi nasema kwa ulkali sana, na nikikuangalia wewe kabisa, nikikwambia maneno ya kweli mbele ya watu hawa wote, wakanye hawa watu wako, kama sivyo wataona cha mtema kuni, na mimi sina mchezo hata kidogo (claps).

Kwa hivyo ndugu zanguni, sisi tunataka usalama katika nchi yetu, sisi tunataka maendeleo katika nchi yetu.

Sisi tunapigana na ukabila, sisi tunapigana na ukabila kabisa, na yeyote atakayeleta ukabila, katika nchi yetu, pahali mngereza atakwenda atamfuata nyuma, akale matako yake. (cheers)

Kwa hivyo sisi tunasema kwamba, nchi ya Kenya haina ukabila, nchi ya Kenya haitatambua mtu yeyote, ambaye anahubiri ukabila.

Sisi tunataka Kenya moja, kutoka pande ya pwani mpaka juu.

Sisi wote ni ndugu moja, sisiI wote ni Wakenya, na nchi yetu ya Kenya itakuwa ni juu yetu kufanya kama tuwezavyo wenyewe kuiendesha.

Part Two.

Kitu gani KPU?! wanasema tume tume kumamazenu! tume.

Wanaleta nini katika Kenya? Wanafanyia nini katika nchi hii ya Wajaluo? Wanafanya nini KPU? twambieni. Kitu gani? Hakuna! Ni mdomo mtupu, kama punda vile analia katika msituni, hakuna kitu kingine.

Lakini serikali yetu tukufu, inafanya mengi kwa wananchi, na itazidi kufanya mengi, kwa wananchi.

Kwa hivyo, mimi nikiwa kiongozi wa serikali hii ya Kenya ninasema, siwezi kukubali, mtu au vikundi vya watu, kuchezea serikali yetu katika ardhi yetu tulioipigania, hapana.

Na kwa hivyo, baada ya kupayuka payuka rafiki yangu nenda fundisha watu wako kulima mashamba yao, wapate faida.

Na wako tayari kama unawafundisha, baada ya kupigapiga kelele huko kelele kule. Kwa hivyo ndugu zanguni, sisi tunataka kuonyesha kwa vitendo.

Uhuru wetu hauwezi kwa midomo mitupu, uhuru wetu ni vitendo, kuonyesha kwa vitendo, tunafanya hii, tunafanya ile, hiyo ndiyo tunataka. Lakini watu wa kupayuka payuka hatutaki Kenya hata kidogo. Tunataka, hii, nchi hii, tulime.

Mimi nilikwenda karibu na kwako wewe bwana Odinga, kule juu, nimekwisha peleka kufyeka misitu huko, kufyeka majani, watu walime.

Na nilipokwenda huko, nilipoangalia angalia, watu wananiambia mzee, watu wanakwisha fyeka, lete majembe ya kulima mashamba haya. Mimi nasema kwa njia mzuri, mimi nitaleta majembe, wanageuka wananiambia mzee, na nani atachimba hii shamba?

Nikawaambia kumamazenu!

Kamahamtumii mikono yenu kuchimba udongo wenu mtoe mali? Basi shauri yenu, msililie serikali.

Kwa hivyo rafiki yangu wafundishe hawa watu wetu, sababu wana akili, wana nguvu ya kuchimba mashamba yao, walime mashamba yao, watoe mali, kuliko kupayuka payuka ovyo ovyo, na wewe uwasaidishe.

Tumefanya na wewe bwana, na hakuna rafiki kuliko wewe, kama ungekuwe wewe ni mtu wa kweli, ujinga? Ungesimama na kusema hiyo mimi nasema ni ukweli.

Sababu hata ndugu yangu mwenyewe, kile nilikupenda wewe, sikumpenda ndugu yangu kama wewe,

(Odinga – ‘lakini mimi iko na chakula cha kutosha’)

Haya, mzuri, kama wewe uko na chakula cha kutosha, vizuri.

(Crowd – ‘sisi iko njaa’)

Ai! Sasa?! Wanakwambia wao wako njaa. Sasa mimi nasema, sababu sikuja hapa tujibiane hivyo, umekubali kama hiyo ni kweli,na kama ni kweli, tufanyie wananchi wetu kazi, baada ya ugomvi ugomvi wa bure.

Baada ya watu yako kutupatupa maneno maneno pale wamepata faida gani?

Wengi watalala ndani ya jela, wengi wamekwisha piga pigwa na askari, walipata faida gani, unafikiri mimi naweza kupenda mambo kama hayo?

(Odinga – wako na njaa)

Kwa nini wewe apana mpe wee chakula?

(Odinga – Eeeh)

Eeh, unashiba, unashibisha tumbo yako na wao unawaacha na njaa, unawaambia kwenda lala! Kwa nini wewe apana wapa chakula? Kama wako na njaa? Baada ya kuja kutupa tupa mawe.

Sasa ndugu zanguni, mimi nasema kwamba, ni lazima, hii nchi yetu ni nchi yetu, na mimi nasema tena hatuwezi kutaka mtu au watu kuharibu nchi yetu.

Hatuwezi kutaka mtu au watu kuharibu uhuru wetu. Umoja wa watu wa Kenya utadumu!

Sababu sisi wote ni ndugu, mbeberu alitaka kututenganisha, akisema huyu ni Mjaluo, huyu ni Mkikuyu, huyu ni Mluhya, huyu ni Mmasai, huyu ni Mkamba, huyu ni…. Sababu katika doctrine yake, katika mipango ya beberu, ni divide and rule, gawanya ndio uweze kutawala.

Labda walikugawia hiyo kitu baba, na wewe unataka kutugawanyagawanya ndio ututawale, hatutakubali hiyo, tunakataa, tunakataa!

(Odinga – wewe ndiye uko na uwezo)

Haya, mimi niko na uwezo, na mimi kama unajua rafiki yangu mimi niko na uwezo, ndio, mimi niko na uwezo, na mimi nitatumia uwezo wangu na njia nzuri, apana kuwaambia kutupatupa mawe pale njiani, njia nzuri, tutafute chakula ya wananchi, tutafute dawa nzuri ya kuwapa watu wetu, kama hospitali hii ambayo wanataka kuiharibu, tutafute dawa nzuri ya kuwatibu.

Tutafute mashule mazuri watu wetu waende wakasome, tufanye mabarabara mazuri watu wetu wapate kwenda katika njia nzuri, na mambo kadhalika.

Tutafute kulima kuzuri ndio wananchi wetu wapate mali kutoka katika udongo wao.

Hiyo ndiyo kazi yetu tukiwa KANU, hiyo ndiyo kazi yetu, na tunawasaidisha wananchi wetu. Na ni lazima tutazidi kuwasaidisha, tutaendelea.

1 просмотр0 комментариев

Недавние посты

Смотреть все

Comments


bottom of page